Mfanyabiashara wa Hong Kong asaidia wanawake wa mitindo ya mavazi wa vijijini kupata maisha yenye ustawi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2023
Mfanyabiashara wa Hong Kong asaidia wanawake wa mitindo ya mavazi wa vijijini kupata maisha yenye ustawi
Zhang Caicai akifanya kazi kwenye kiwanda huko Yinchuan, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini Mashariki mwa China, Machi 3, 2023. (Xinhua/Ai Fumei)

YINCHUAN - Huku kukiwa na  mistari ya uzalishaji na  vyerahani vya kushona kwa kasi, wafanyakazi wengi wanawake wanashughulika  kushona pamoja nguo katika kiwanda, wakitengeneza bidhaa za nguo za ndani huku wakitimiza ndoto yao ya kujenga maisha bora.

Miaka mingi iliyopita, wengi wao walikuwa bado ni mama wa nyumbani katika maeneo ya vijijini katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia nchini China. Wakati huo, kupata mshahara mzuri huku wakiweza kutunza familia zao ilionekana kuwa jambo lisilowezekana.

Hata hivyo, tangu kuwasili kwa kiwanda karibu na jumuiya yao miaka minne iliyopita, mambo yamebadilika sana.

Mwaka 2019, Benny So, mfanyabiashara kutoka Hong Kong, aliamua kuhamisha sehemu ya uzalishaji wa kampuni yake yenye makao yake katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao ya China kutoka Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China hadi Kijiji cha Xinrong katika Wilaya ya Helan ya Ningxia.

Kuanzisha kiwanda mkoani Ningxia, ambayo ni kituo kikuu cha Mpango wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kulimaanisha kuwa bidhaa hizo zingeweza kufikia soko la Ulaya haraka zaidi kupitia treni za mizigo   zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya. Ikilinganishwa na usafirishaji wa baharini, treni za mizigo za kati ya China na Ulaya zinaweza kupeleka bidhaa wanazozizalisha za nguo za ndani za kiwango cha juu hadi Ulaya ndani ya nusu ya muda.

"Kwa bidhaa za mitindo ya mavazi zinazozingatia wakati, ufanisi wa usafirishaji ni muhimu," amesema Mfanyabiashara So mwenye umri wa miaka 63.

Bado anakumbuka kwamba katika ziara yake ya kwanza katika kijiji hicho, viongozi wa eneo hilo walisema kiwanda hicho kitakuwa mradi wa kupunguza umaskini unaotoa ajira kwa wakazi waliohamishwa kutoka Xihaigu, eneo ambalo hapo awali lilichukuliwa kama "lisilofaa kuishi kwa watu."

"Nadhani itakuwa vyema kuleta mapato zaidi kwa wakazi maskini," amesema, huku akiongeza kuwa wafanyakazi katika kiwanda hicho wanapata wastani wa yuan 5,000 (kama dola 724 za Marekani) hadi yuan 6,000 kwa mwezi.

Zhang Caicai, mmoja wa wafanyakazi wa kwanza katika kiwanda hicho, anasema alikuwa akipata kazi zisizo za kawaida ambazo zilikuwa za kuchosha na zinazomlipa ujira mbaya.

"Nikiwa na kazi hii karibu na nyumbani, ninaweza kuangalia na kutunza familia yangu bila kulazimika kumuomba mume wangu pesa," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha