Maandamano ya kupinga vita yafanyika Kusini mwa California baada ya miaka 20 kupita tangu Marekani kuivamia Iraq

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2023

Mwandamanaji akionekana mbele ya Kituo cha Ndege cha Marine Corps Miramar, umbali wa kilomita 25 Kaskazini mwa jiji la San Diego, California, Marekani, Machi 18, 2023. (Picha na Zeng Hui/Xinhua)

SAN DIEGO, Marekani - Mashirika ya kupinga vita yamefanya maandamano huko Los Angeles na San Diego siku ya Jumamosi katika kuelekea kumbukumbu ya miaka 20 tangu uvamizi wa Marekani nchini Iraq, ulioanza Machi 20, 2003.

Maandamano hayo yanakuja wakati ambapo kuna maandamano ya kitaifa ya kupinga vita yaliyoandaliwa na Asasi ya Chukua hatua Sasa Kukomesha Vita na Kukomesha Ubaguzi wa Rangi (Mungano wa ANSWER), asasi ambayo ni mwavuli wa maandamano yenye makao yake makuu nchini Marekani inayojumuisha mashirika mengi ya kupinga vita na yale ya utetezi wa haki za kiraia.

"Tuliona leo ni hatua nzuri ya kujumuika na vijana kujadili masuala yanayohusika. Inakumbuka kutimia kwa miaka 20 ya uvamizi wa Marekani nchini Iraq," Gary Butterfield, mwanajeshi mkongwe mstaafu, ameliambia Shirika la Habari la Xinhua.

Wakiwa wamenyanyua mabango yenye maandishi yanayosomeka "Pesa mahitaji ya watu, siyo mashine ya vita," "Jenga shule siyo mabomu," "Njia ya amani nchini Ukraine: Zungumza, Usichochee," "Kwa amani: Vunja NATO" na baadhi ya waandamanaji hao walikusanyika mbele ya lango la Kituo cha Ndege cha Marine Corps Miramar, umbali wa kilomita 25 Kaskazini mwa Jiji la San Diego.

Waandamanaji hao pia walipiga sauti wakisema "Pesa kwa kazi na elimu, siyo kwa vita na uvamizi" na madereva wengi waliokuwa wakipita njiani walipiga honi kuonyesha uungaji mkono.

Butterfield amesema Serikali ya Marekani inapaswa kuelekeza fedha kwenye masuala ya maendeleo kama vile huduma za afya, matunzo ya watoto na elimu badala ya vita na mashindano ya silaha.

Kuhusu msukosuko wa Ukraine, ambao umepamba moto mwaka mmoja uliopita, Butterfield amesema: "Maisha ya watu wengi sana yanapotea, na kunapaswa kutiliwa mkazo zaidi katika diplomasia na mazungumzo."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha