

Lugha Nyingine
Uwezo wa China wa kuzalisha nishati mbadala waongezeka katika kipindi cha Miezi ya Januari na Februari Mwaka 2023
![]() |
Picha hii iliyopigwa Tarehe 7 Februari 2023 ikionyesha eneo la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua ulioko Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Sun Fanyue) |
BEIJING, - Uwezo wa mitambo ya kuzalisha nishati mbadala iliyofungwa nchini China ulipata ukuaji mkubwa katika miezi miwili ya kwanza ya Mwaka 2023, takwimu rasmi kutoka Idara ya Kitaifa ya Nishati ya China zimeonyesha Jumanne.
Mwishoni mwa Februari, uwezo wa mashine zilizofungwa za kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya upepo uliongezeka kwa asilimia 11 kuliko mwaka jana hadi kufikia umeme wenye nguvu za takribani kilowati milioni 370, wakati ule unaotokana na nishati ya jua umefikia karibu nguvu ya kilowati milioni 410, ikionesha ongezeko kubwa la asilimia 30.8 kuliko mwaka uliopita.
Jumla ya uwezo wa mashine zilizofungwa za kuzalisha umeme nchini China ilifikia uzalishaji wa umeme wenye nguvu ya takriban kilowati bilioni 2.6 hadi kufikia mwisho wa Februari, ikiwa ni kuongezeka kwa asilimia 8.5 kuliko mwaka uliopita.
China imeongeza uwekezaji wake wa nishati mbadala kwa miaka mingi ili kufuata maendeleo ya kijani.
Katika miezi miwili ya kwanza, uwekezaji wa jumla wa makampuni makubwa ya umeme ya China katika nishati ya jua uliongezeka karibu mara tatu kuliko mwaka uliopita hadi yuan bilioni 28.3 (kama dola za Marekani bilioni 4.12), takwimu hizo zimeonyesha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma