Xi na Putin wasaini taarifa ya pamoja ya Kuimarisha Uhusiano Wenzi wa Kimkakati wa Pande zote wa Uratibu Katika Zama Mpya

(CRI Online) Machi 22, 2023

(Picha inatoka shirika la Habari la China Xinhua.)

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin Jumanne katika Ikulu ya Kremlin wamesaini na kutoa taarifa ya pamoja ya marais juu ya Kuimarisha Uhusiano Wenzi wa Kimkakati wa Pande zote wa Uratibu Katika Zama Mpya.

Kwenye taarifa hiyo, pande hizo mbili zimesema uhusiano wa China na Russia sio kama ule wa muungano wa kijeshi na kisiasa wakati wa vita baridi, bali unaenda mbali zaidi katika uhusiano wa serikali na serikali na una asili ya kutokuwa wa muungano, kutokuwa wa mapambano na kutolenga upande wowote wa tatu. Zimesema kuwa nchi mbalimbali zina historia, tamaduni na hali tofauti za kitaifa, na zote zina haki ya kuchagua njia zao za maendeleo. Hakuna kitu kama "demokrasia" bora zaidi.

Kwenye taarifa hiyo Russia imethibitisha kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, kuitambua Taiwan kuwa eneo lisiloweza kutengwa la China, kupinga aina yoyote ya Kujitenga kwa Taiwan na kuunga mkono kithabiti hatua za China za kulinda mamlaka na ukamilifu wake wa ardhi.

Halikadhalika pande hizo mbili pia zimeeleza wasiwasi wao mkubwa kuhusu shughuli za silaha za kibaolojia za Marekani, ndani na nje ya nchi hiyo, ambazo zinatishia kwa kiasi kikubwa nchi nyingine na kudhoofisha usalama wa kanda husika. Hivyo wameitaka Marekani kutoa maelezo juu ya suala hili, na kujizuia kuendeleza shughuli zozote za silaha za kibaolojia ambazo zinakiuka Mkataba wa Silaha za Kibaolojia.

Pande hizo mbili pia zimeitaka Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) kufuata ahadi zake za kuwa jumuiya ya kikanda na ya kujilinda, na kuitaka kuheshimu mamlaka, usalama, maslahi pamoja pia na ustaarabu mbalimbali, historia na utamaduni wa nchi nyingine, na kuchukulia maendeleo ya amani ya nchi husika kwa njia sahihi na ya haki. Pia zimeelezea wasiwasi wao mkubwa juu ya NATO kuendelea kuimarisha uhusiano wa ulinzi wa kijeshi na nchi za Asia na Pasifiki na kudhoofisha amani na utulivu wa kanda hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha