Timu ya madaktari wa China yasifiwa kwa kutoa huduma za afya Sudan Kusini

(CRI Online) Machi 24, 2023

Timu ya 10 ya madaktari wa China imesifiwa kwa kutoa huduma za matibabu kwa zaidi ya watu 2,000 wanaoishi karibu na uwanda wa mafuta wa Paloch katika Kaunti ya Melut, Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini.

Kamishna wa Kaunti hiyo, Deng Jok Angok ameipongeza timu hiyo kwa kutoa ushauri na matibabu bila malipo kwa makundi maalum ya raia ambao wanaitegemea Hospitali ya Urafiki ya Paloch kupata huduma za afya.

Amesema wakazi wengi wa kaunti hiyo ni masikini na mara nyingi inakuwa vigumu kwao kusafiri kwenda kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kwa ajili ya matibabu, na kuongeza kuwa, ziara ya timu za madaktari wa China kuanzia tarehe 5 hadi 18 mwezi huu imebadili maisha yao.

Kiongozi wa timu hiyo ya madaktari wa China, Xu Zhangwei amesema, wafanyakazi wenzake pia wanabadilishana uzoefu wao wa kitabibu na wafanyakazi wazawa katika Hospitali ya Urafiki ya Paloch, iliyojengwa na Shirika la Mafuta la China (CNPC).

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha