Sekta ya Kilimo cha Pamba ya China kuendeleza maendeleo yenye ubora wa juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 24, 2023

Mashine ya kuchuma pamba ikifanya kazi kwenye shamba la pamba katika Wilaya ya Xayar, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha na Liu Yuzhu/Xinhua)

BEIJING – Sekta ya kilimo cha pamba ya China itaendelea kuboresha sifa ya utoaji wa pamba ili kuchochea mahitaji ya soko na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu, Shirikisho la Ushirika wa Utoaji na Uuzaji wa Mazao la China limesema siku ya Alhamisi.

“China ni mzalishaji, muagizaji na mtumiaji mkubwa zaidi wa pamba duniani, vilevile ni muuzaji mkubwa kwenye soko la kimataifa la bidhaa za nguo” amesema Hou Shunli, Naibu Mkurugenzi wa baraza la shirikisho hilo kwenye mkutano wa mwaka wa sekta ya kilimo cha pamba.

Hou amehimiza kufanya juhudi za kuendeleza uvumbuzi wa bidhaa, kupanua mahitaji ya ndani, na kutumia teknolojia za kidijitali kwenye viungo vyote vya mnyororo wa sekta ya kilimo cha pamba ili kuharakisha uboreshaji wa sekta hiyo.

“Juhudi pia zinapaswa kufanywa ili kuongeza kwa kufaa maeneo ya uzalishaji wa pamba, kuhakikisha utoaji wa malighafi kwenye sekta ya nguo, na kuendelea kuboresha uthabiti na usalama wa mnyororo wa viwanda na utoaji wa malighafi ” Hou amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha