Sekta ya mawasiliano ya simu ya China yapata upanuzi thabiti katika miezi ya Januari na Februari, 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 24, 2023

Watu wakitembelea banda la maonyesho la Shirika la Simu la China, China Telecom kwenye Mkutano wa Dunia wa Teknolojia ya 5G Mwaka 2022 huko Harbin, Mji Mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Agosti 10, 2022. (Xinhua/Zhang Tao)

BEIJING - Takwimu kutoka Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China zinaonyesha kuwa, Sekta ya mawasiliano ya China imepata upanuzi thabiti katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu wa 2023, ikiwa na upanuzi mkubwa wa biashara zinazoibukia na miundombinu mipya.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, mapato ya biashara ya kampuni zinazojihusisha na sekta hiyo yalifikia yuan bilioni 280.3 (kama dola bilioni 40.8 za Kimarekani), ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.9 kutoka kwenye kiwango cha mwaka jana.

Kwa jumla, sekta zinazoibuka kama vile vituo vya data vya mtandao, mifumo ya kompyuta wingu na Mambo ya Mtandao zilishuhudia mapato yao yakipanda kwa asilimia 25.7 kutoka kwenye kiwango cha mwaka jana, na kuwezesha mapato yatokanayo na biashara ya mawasiliano ya simu kuongezeka kwa asilimia 5, wizara hiyo imesema.

Takwimu hizo pia zinaonyesha maendeleo thabiti ambayo China imepata katika kuendeleza ujenzi wa miundombinu mipya. China ilikuwa na vituo vya msingi vya teknolojia ya 5G milioni 2.38 kufikia mwisho wa Februari mwaka huu, yaani vituo 72,100 zaidi kutoka kwenye idadi iliyokuwepo mwishoni mwa mwaka jana wa 2022.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha