Mauzo ya magari yaliyotumika nchini China yaripoti upanuzi mkubwa Mwezi Februari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2023
Mauzo ya magari yaliyotumika nchini China yaripoti upanuzi mkubwa Mwezi Februari
Magari yakiendeshwa kwenye Barabara ya Lianshi Mashariki wakati wa pilika za watu wengi kwenda kazini asubuhi hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Januari 3, 2023. (Xinhua/Zhang Chenlin)

BEIJING - Mauzo ya magari yaliyotumika nchini China yamerekodi kuimarika tena kwa nguvu Mwezi Februari, kwa kuchochewa na kuongezeka kwa mahitaji ya manunuzi na ufufukaji mkubwa wa soko baada ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, takwimu za Shirikisho la Wafanyabiashara wa Magari la China zinaonesha.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, katika mwezi uliopita, takriban magari milioni 1.46 yaliyotumika yaliuzwa kote nchini China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 35.48 kuliko yale ya kipindi kama hicho mwaka jana.

Katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, zaidi ya magari milioni 2.7 yaliyotumika yaliuzwa nchini China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.68 kuliko yale ya kipindi hicho cha mwaka uliopita.

Shirikisho hilo limesema, “Soko la magari yaliyotumika lilipata nguvu kubwa tena Mwezi Februari, na mahitaji ya awali yataendelea kuleta fursa kubwa kwenye soko,” na sera mpya ya China ya kuhimiza shughuli za biashara kubwa na zenye viwango katika sekta hiyo itahimiza maendeleo yenye ubora ya soko.

Shirikisho hilo limeeleza matumaini yake kuhusu matarajio ya siku za baadaye ya soko hilo na limebainisha kuwa kadri kampuni za magari yaliyotumika zinaporejea kujiamini, soko linatarajiwa kupata ufufukaji taratibu.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha