Alama za utamaduni wa China kwenye medali za Mashindano ya mbio za Marathon

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2023

Katika miaka ya hivi karibuni, mashindano ya mbio za Marathon yanafanyika mara kwa mara katika sehemu mbalimbali nchini China na kuvutia ufuatiliaji na ushiriki wa watu wengi zaidi. Usanifu wa medali nyingi za mashindano hayo umehusisha alama za utamaduni wa China, zikionesha mvuto wa kipekee wa utamaduni wa jadi wa China. Medali hizo siyo tu zimewapa wanariadha fahari, bali pia zimekuwa ni kadi za miji inayoandaa mashindano hayo. Medali ndogo huhusisha utamaduni na kumbukumbu za mji mmoja.

1.Medali za Mashindano ya Mbio za Marathon ya Suzhou 2023

Picha kutoka kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa wechat wa “Suzhou Marathon ”.

Usanifu wa medali hiyo ulitokana na madirisha yanayojulikana yenye umbo la Maua ya Begonia katika Bustani za Suzhou. Michongo juu yake ilitokana na picha zenye mtindo pekee uliobuniwa na msanifu kwa kuashiria sura ya “Mfereji Mkuu” maarufu wa China, hali ambayo imeonesha muunganiko wa mvuto wa utamaduni wa jadi wa China na mtindo wa kisasa.

2.Medali za wakimbiaji waliokamilisha mbio za Marathon za Shell Beijing 2022

Picha kutoka kwenye tovuti ya Beijing Marathon.

Usanifu wa Medali hiyo unaonesha sehemu yalipoanzia mashindano ya mbio za marathon kwenye Uwanja wa Tian’anmen, alama maarufu ya Jiji la Beijing, na kuongeza muundo wa kuvutia wa “lango” linaloweza kufunguliwa na kufungwa la Jengo la Tian An Men . Kwenye upande wa kulia wa lango hilo, kuna kaligrafia ya Kichina ya “Beijing Marathon”; na mchongo wa “dragon anayerukaruka kama aliye hai” unaonekana kwenye nguzo ya kila upande wa lango hilo.

3.Medali za Mashindano ya Mbio za Marathon ya Wuxi 2023

Picha kutoka tovuti ya Wuxi Marathon.

Sehemu iliyobonyea ya nusu ya juu ya medali ni kama ziwa lenye maji safi, na majani ya maua ya yungiyungi na maua ya cherry yanaelea kimya kimya kwenye ziwa. Upande wa nyuma wa medali hiyo kuna mchongo wa ndege phoenix anayependeza, usanifu huu unatokana na sanaa ya kale ya jade ya Dola ya Yue ya “Phoenix Anayeruka” iliyofukuliwa huko Wuxi, ikiwakilisha hali nzuri ya Wuxi ya kurithisha historia na utamaduni.

4. Medali za wakimbiaji waliokamilisha mbio za Marathon za Chengdu 2022

Picha kutoka Chinanews na zimetolewa na Idara ya Michezo ya Mji wa Chengdu.

Usanifu wa medali hii ukionesha sanaa ya “maua ya dirishani” katika utamaduni wa jadi wa China, sehemu iliyo wazi kwenye medali hiyo inawawezesha watu kupata taswira ya maono ya ngazi, na juu yake pia kuna mchongo wa sura ya ndege wa jua wa ajabu, kwa kuashiria hali ya uhai ya mji wa Chengdu.

5.Medali za wakimbiaji waliokamilisha Mbio za Marathon za Mlango wa Mto Manjano 2021

 

Picha kutoka kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa wechat wa Mbio za Marathon za Mlango wa Mto Manjano.

Usanifu wa Medali hiyo ya umbo usio wa kawaida, unaoonyesha mtiririko mwororo wa maji ya mto kwenye "Mlango wa Mto Manjano". Sehemu ya mbele ni michongo ya ardhi oevu na maeneo ya mafuta, ikionyesha vilivyo sifa ya mji wa Dongying; na michongo ya ndege wanaoruka juu inamaanisha binadamu kuishi katika hali ya mapatano na mazingira ya asili.

6. Medali za wakimbiaji waliokamilisha Mbio za Marathon za Guangzhou 2020

Picha kutoka tovuti rasmi ya Guangzhou Marathon.

Usanifu wa medali hii inaonesha sura ya Simba--uwakilishi wa utamaduni wa Lingnan kwa kuashiria moyo wa kujikakamua bila kulegalega, na sura ya simba mwenye hekima na ushujaa huwahimiza watu waungane na kuwa na ari kubwa. Sehemu ya nje ya medali imeundwa kwa michongo ya mawimbi kwa kuashiria wakimbiaji wanakimbia bila kusita wakiwa wanakabiliwa na upepo na mawimbi kwenye njia za mashindano ya mbio.

7. Medali za Wakimbiaji waliokamilisha Mbio za Marathon za Shaoxing Yuema 2020

 

Picha inatoka kwenye tovuti ya Shaoxing.

Medali hiyo imesanifiwa kwenye msingi wa muundo wa kofia aliyovaa ofisa Wang Yangming na mabaki ya kale ya “Kioo cha Shaba cha mji wa kale wa Kuaiji”. Nusu ya juu ya upande wa mbele wa medali hiyo imeunganisha nembo ya mashindano hayo na fikra ya Wang Yangming ya “muunganiko wa ujuzi na vitendo”. Nusu ya chini ya upande wa mbele wa medali hiyo imeonesha maana ya “Kioo cha Shaba cha Kuaiji” inayoendana na fikra ya Wang Yangming.

8. Medali za kumaliza mbio za Marathon za Kimataifa za Lanzhou 2019

Picha kutoka kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa wechat wa “Lanzhou Marathon ”.

Usanifu wa medali hiyo unatokana na umbo la gurudumu la maji la Lanzhou. Michongo kwenye duara ya nje ya medali inatokana na vigae kauri vya rangi vya Majayao huko Lanzhou. Kwenye duara ya ndani ya medali, lina mchongo wa gurudumu la maji linaloweza kuzungushwa, na chini yake ni michongo ya mawimbi yanayoashiria utamaduni wa Mto Manjano wenye nguvu ya uhai usio na mwisho, na kuonyesha historia ndefu ya utamaduni wa mji wa Lanzhou ulioko kando ya Mto Manjano unaotiririka kwa kasi daima.

9.Medali za wakimbiaji wa kukamilisha nusu mbio kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Mbio za Marathon ya Jianzhen ya Yangzhou 2019

Picha kutoka kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa wechat wa ”Yangzhou Marathon ”.

Usanifu wa medali hiyo ni mchongo wa "Daraja la Wanfu" la Yangzhou, ambalo ujenzi wake unaunganisha mtindo wa kisasa na kijadi. Kwenye upande wa nyuma wa medali hiyo, kuna mchongo wa mawimbi ya maji, unaoashiria maji ya Mfereji Mkuu yanayotiririka bila kusita ambayo yamelea Mji wa Yangzhou kwa maelfu ya miaka.

10.Medali za Mashindano ya Mbio za Marathon ya Hangzhou 2017

Picha kutoka kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa wechat wa “Hangzhou Marathon ”.

Mbele ya medali hii ni mchongo wa muhuri wenye maandiko ya kaligrafia“Hangzhou Marathon 2017”. Muhuri huo wa awali ulichongwa na msanii wa kitaifa wa daraja la kwanza Bw. Wu Ying, ambaye ni mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mihuri la Xiling, msanifu wa medali alinukuu uchongaji wa muhuli huo kwenye Medali hiyo na kuifanya medani kuwa muhuri kweli pia, hivyo medali hii imekuwa na thamani ya juu ya kisanii na ya kuhifadhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha