China yaahidi kuendeleza demokrasia ya kijamaa na uhusiano wa pande mbili na Vietnam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2023

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Spika wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Vietnam Vuong Dinh Hue kupitia njia ya video kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 27, 2023. (Xinhua/Liu Weibing)

BEIJING - China Jumatatu imeahidi kushikilia na kuendeleza demokrasia ya kijamaa pamoja na Vietnam, na kuimarisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Vietnam katika zama mpya.

Zhao Leji alitoa ahadi hiyo alipofanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Vietnam Vuong Dinh Hue kwa njia ya video.

Zhao Leji ameeleza kuwa China na Vietnam ni marafiki jirani wenye kufuata mfumo wa kijamaa. Amesema China iko tayari kushirikiana na Vietnam ili kuimarisha urafiki wa jadi, kufuata mwongozo wa kimkakati wa kiwango cha juu, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuboresha zaidi ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha uungaji mkono wa umma kwa urafiki kati ya nchi hizo mbili, kujitolea kufuata njia ya ujamaa inayoendana na hali za nchi husika, na kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja ambao una umuhimu wa kimkakati.

Ametoa wito kwa Bunge la Umma la China na Bunge la Vietnam kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya kamati maalum, makundi ya urafiki, wajumbe na vyombo vya mabunge ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Hue, ambaye ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, amesema Vietnam inatilia maanani kuendeleza uhusiano na China kama chaguo la kimkakati na kipaumbele cha juu cha sera yake ya nje na inaheshimu na kufuata kwa dhati sera ya kuwepo kwa China moja.  

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Spika wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) akifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Vietnam Vuong Dinh Hue kupitia njia ya video kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Machi 27, 2023. (Xinhua/Liu Weibing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha