Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Tanzania asema kanuni za China kuhusu uhusiano na Afrika ina maadili ya pamoja kwa pande zote mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2023

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Tanzania Vita Kawawa akizungumza kwenye kongamano jijini Dar es Salaam, Tanzania Machi 24, 2023. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

DAR ES SALAAM - Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Tanzania Vita Kawawa amesema misingi ya China ya uaminifu, matokeo halisi, mshikamano na imani njema, pamoja na kujitolea kwake kwa maslahi makubwa zaidi na ya pamoja siyo tu ni kanuni na maono ya kuendeleza uhusiano na nchi za Afrika, bali pia ni maadili ya pamoja ya Afrika na China.

Kawawa aliyasema hayo alipohudhuria kongamano la maadhimisho ya miaka 10 tangu Rais Xi Jinping wa China afanye ziara ya kiserikali nchini Tanzania na kuanzishwa kwa kanuni na dhamira zilizotajwa hapo juu. Kongamano hilo lililofanyika liliandaliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania.

“Chini ya mwongozo wa kanuni na dhamira, China na Tanzania zimefanya ushirikiano wenye tija, na kuleta manufaa yanayoonekana kwa Tanzania,” Kawawa amesema, huku akielezea matarajio yake kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili utapata maendeleo makubwa, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi zote mbili.

Maofisa wengine wa Tanzania waliohudhuria kongamano hilo pia wameeleza kuwa kanuni na dhamira hizo zinathibitisha kuwa China ni rafiki wa dhati ambaye nchi za Afrika zinaweza kumwamini na kumtegemea.

Chen Mingjian, Balozi wa China nchini Tanzania, alifafanua maana ya msingi, thamani, umuhimu wa kihistoria, utendaji na mafanikio ya kanuni hizo za China katika uhusiano wake na Afrika.

“China iko tayari kushirikiana na Tanzania kutekeleza kwa pamoja Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, na kukuza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Tanzania kuelekea siku nzuri za baadaye.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha