Hospitali inayosaidiwa na China nchini Zimbabwe yaleta ahueni ya matibabu kwa wenyeji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 29, 2023

Wanakijiji wakiwa wamesimama kwenye bango linaloelekeza njia ya kwenda Hospitali ya Mahusekwa ya Jimbo la Mashonaland Mashariki, Zimbabwe, Tarehe 24 Machi, 2023. (Xinhua/Zhang Baoping)

MAHUSEKWA, Zimbabwe - Hospitali inayofadhiliwa na China katika maeneo ya vijijini ya Zimbabwe inaleta msaada kwa wanavijiji ambao walikuwa wakivumilia kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.

Hospitali ya Mahusekwa, ambayo pia inajulikana kama Hospitali ya Urafiki wa China na Zimbabwe, ilijengwa kwa msaada wa China ili kutoa huduma bora za afya huko Mahusekwa, eneo la vijijini katika Wilaya ya Marondera, Mashariki ya Harare.

Ujenzi wa kipindi cha kwanza wa Mradi wa Hospitali ya Mahusekwa ulikamilika na kukabidhiwa kwa serikali ya Zimbabwe Mwaka 2012. Ujenzi wa kipindi cha pili wa Mradi huo ulianzia Mwaka 2019, eneo lake la jumla ni mita za mraba 5,220, kwenye eneo hilo kuna ua mkubwa na vifaa vilivyoboreshwa kwenye chumba cha kuhifadhia miili, chumba cha kuua viini, na chumba cha kufulia nguo, miongoni mwa vingine.

Hospitali hiyo ya kisasa ina wodi za kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa meno, watoto, ukumbi wa michezo, radiolojia na ukandaji wa mwili, chumba cha kuhifadhia miili, na cha akina mama wajawazito, kati ya zingine.

Ofisa wa Matibabu wa Wilaya ya Marondera, Delight Madoro amesema hospitali hiyo imeleta urahisi mkubwa katika matibabu ya wagonjwa.

"Mahusekwa iko mbali kidogo na mji mkuu wa jimbo wa Marondera pamoja na Harare. Kabla ya kujengwa na kufunguliwa kwa hospitali hiyo, watu walikuwa wakienda Marondera au Harare kutafuta huduma za matibabu, lakini tangu kufunguliwa kwa hospitali hiyo, watu wanaweza kupata huduma bora za afya na kwa urahisi katika wilaya hiyo," Madoro ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Amesema hospitali hiyo imeleta mabadiliko makubwa, kwani wenyeji na hata watu kutoka maeneo ya mbali ya Harare, ambayo yako umbali wa zaidi ya kilomita 100, hufika kupata matibabu.

"Kwa maoni yangu, msaada huu kutoka China kwa huduma zetu za afya ni muhimu sana kwa vile bado tunaendelea kupata msaada kutoka Jamhuri ya Watu wa China. Msaada huu unakuja katika mfumo wa nguvu kazi. Pia unakuja katika mfumo wa vifaa na matumizi mbalimbali katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa wetu," Madoro amesema.

Serikali ya Zimbabwe inalenga kutoa huduma ya afya kwa wote ifikapo Mwaka 2030, na China imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha mfumo wa huduma za afya nchini humo.

China na Zimbabwe zimefanya ushirikiano kwa muda mrefu katika sekta ya afya. Tokea Mwaka 1985, China imekuwa ikituma timu za madaktari nchini Zimbabwe.

Mwendesha baiskeli akiingia katika Hospitali ya Mahusekwa ya Jimbo la Mashonaland Mashariki, Zimbabwe, Machi 24, 2023. (Xinhua/Zhang Baoping)

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Marondera, Delight Madoro (kushoto) akimkagua mtoto mchanga kwenye mashine ya kuatamia mtoto mchanga katika Hospitali ya Mahusekwa ya Jimbo la Mashonaland Mashariki, Zimbabwe, Machi 24, 2023. (Xinhua/Zhang Baoping)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha