Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Malaysia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 29, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia Zambry Abd Kadir mjini Beijing, China, Machi 28, 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amefanya mazungumzo na mwenzake wa Malaysia Zambry Abd Kadir mjini Beijing siku ya Jumanne.

Kwenye mazungumzo hayo Qin amesema, China na Malaysia, zikiwa nchi zinazoendelea na nchi muhimu zinazoibukia kiuchumi barani Asia na zenye nguvu muhimu katika ngazi ya kimataifa, zinapaswa kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha urafiki, kushirikiana pamoja ili kukabiliana na hatari na changamoto, na kuchangia zaidi kwa amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kikanda na kimataifa.

Qin ametoa wito kwa pande zote mbili kuharakisha miradi muhimu na kutafuta fursa mpya za ushirikiano zaidi katika maeneo kama vile magari yanayotumia nishati mpya, uchumi wa kidijitali, semiconductor na kilimo.

Kwa upande wake Zambry Abd Kadir amesema ziara rasmi ijayo ya Waziri Mkuu wa Malaysia Datuk Seri Anwar Ibrahim nchini China itaendeleza urafiki wa nchi hizo mbili kwenye kiwango cha juu zaidi.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Malaysia amesema Malaysia iko tayari kushirikiana na China ili kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa kikanda na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya karibu ya China na ASEAN yenye mustakabali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha