China Bara yathibitisha kuwepo kwa manufaa halisi kwa watu wa Taiwan baada ya kutimiza Muungano wa Taifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2023

Zhu Fenglian, Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari hapa Beijing, China, Machi 29, 2023. (Xinhua/Chen Yehua)

BEIJING - Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China siku ya Jumatano amethibitisha kuwa watu wa Taiwan watafurahia manufaa halisi baada ya kutimiza Muungano wa Taifa.

Zhu amesema kuwa baada ya kutimiza Muungano wa Taifa, Taiwan inaweza kufuata mfumo wa kijamii tofauti na ule wa China Bara.

Ameongeza kuwa, isipokuwa kwamba mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo ya China yanahakikishwa, mfumo wa kijamii wa Taiwan na mtindo wake wa maisha utaheshimiwa kikamilifu, na mali binafsi, imani za kidini, haki na maslahi halali ya watu wa Taiwan yatalindwa kikamilifu.

Pia amesema baada ya kutimiza Muungano wa Taifa, mfumo na muundo wa ushirikiano wa kiuchumi wa Mlango Bahari utaboreshwa zaidi, ubunifu wa utamaduni wa kisiwa hicho unatarajiwa kuwa thabiti zaidi, na watu wa Taiwan watapata fursa zaidi za maendeleo katika dunia. 

Zhu Fenglian, Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, akionyesha ishara katika wakati wa maswali na majibu kwenye mkutano na waandishi wa habari, Machi 29, 2023. (Xinhua/Chen Yehua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha