Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kutaka ufafanuzi wa mahakama kuhusu wajibu wa mabadiliko ya tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2023

Picha iliyopigwa Septemba 14, 2020, ikionyesha mwonekano wa nje wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. (Xinhua/Wang Ying)

UMOJA WA MATAIFA - Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumatano limepitisha azimio la kutafuta maoni ya chombo kikuu cha mahakama cha jumuiya hiyo ya Dunia kuhusu wajibu wa nchi kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

Azimio hilo, lililotolewa na Nchi ya kisiwa ya Vanuatu na kupitishwa kwa makubaliano, linataka maoni ya ushauri usiyolazimisha wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu wajibu wa mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi.

Maswali ambayo ICJ inapaswa kufafanua ni pamoja na "ni wajibu gani wa mataifa chini ya sheria ya kimataifa katika kuhakikisha ulinzi wa mfumo wa tabianchi na maeneo mengine ya mazingira kutokana na utoaji wa hewa zinazochafua mazingira," kwa mujibu wa azimio hilo.

Azimio hilo pia linaonyesha wasiwasi mkubwa kwamba lengo la nchi zilizoendelea la kukusanya kwa pamoja dola za Kimarekani bilioni 100 kwa mwaka ifikapo Mwaka 2020 "katika muktadha wa hatua za maana za kupunguza athari za tabianchi na uwazi wa utekelezaji" bado halijafikiwa, na linazitaka nchi zilizoendelea kufikia lengo.

Katika hotuba yake kwa Baraza Kuu kabla ya upigaji kura, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alielezea matumaini yake kwamba maoni ya ushauri wa ICJ yanaweza kutoa ufafanuzi juu ya wajibu uliopo wa kisheria wa kimataifa. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha