Timu ya madaktari wa China nchini Rwanda yatoa huduma ya kliniki bila malipo katika hospitali ya nchi hiyo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2023
Timu ya madaktari wa China nchini Rwanda  yatoa huduma ya kliniki bila malipo katika hospitali ya nchi hiyo
Madaktari wa China wakifanya upimaji wa afya kwa wenyeji mjini Kigali, Rwanda, Machi 27, 2023. (Xinhua/Ji Li)

KIGALI - Timu ya 23 ya Madaktari wa China iliyotumwa Rwanda imetoa huduma ya kliniki bila malipo katika Hospitali ya Masaka iliyopo Kigali, Mji Mkuu wa Rwanda, katika kuadhimisha Wiki ya Matibabu kwa kutumia Ganzi ya China ambayo ni shughuli ya kila mwaka.

Katika shughuli hiyo Jumatatu, madaktari wa China na madaktari wa Rwanda pia walifanya mkutano kwa njia ya mtandao kuhusu Matibabu kwa kutumia Ganzi na madaktari kutoka Hospitali ya Umma ya Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China ili kubadilishana mawazo na mbinu bora za kutumia matibabu ya ganzi na kudhibiti maumivu wakati wa taratibu za upasuaji.

Kliniki hiyo ya bila malipo imetoa huduma za matibabu yanayohitajika sana kwa wale ambao labda vinginevyo wasingeweza kuipata. Mamia ya wagonjwa wa eneo hilo walikwenda kliniki hiyo ya bila malipo, ambapo walipata huduma ya matibabu, ikiwa ni pamoja na kupima shinikizo la damu, upimaji wa glukosi na kolesteroli, pamoja na mashauriano na wataalamu wa afya kuhusu matatizo yao ya kiafya.

"Tumeadhimisha Wiki ya Matibabu kwa Kutumia Ganzi ya China kwa lengo la kutoa elimu kwa wenyeji nchini Rwanda juu ya aina mbalimbali za upasuaji wa kutumia ganzi na jinsi ya kukabiliana na maumivu hasa kwa akina mama walio katika hatua ya kujifungua na wanaofanyiwa upasuaji. Hii itawasaidia kwa ufanisi kupunguza maumivu kwa kiasi kikubwa," Zhao Shangjun, Mkuu wa Timu ya Madaktari wa China, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano.

Amesema kliniki hiyo ya bila malipo iliwapokea wagonjwa wa eneo hilo ambao walipimwa afya zao kwa ujumla na kubainishwa hatari zinazowezekana za magonjwa ambayo kabla ya hapo hawakujua wanayo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha