IOM yatoa wito kwa nchi za Afrika kuchochea uchumi kwa kuruhusu uhamiaji wa nguvukazi zenye ujuzi

(CRI Online) Machi 31, 2023

Shirikisho la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema nchi za Afrika zinapaswa kutunga sera na kanuni za kisheria zinazowezesha safari za kuvuka mipaka kwa nguvukazi zenye ujuzi ili kuchochoea ukuaji wa kiuchumi, utulivu na mshikamano.

Mkurugenzi wa Ofisi ya IOM Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Mohammed Abdiker amesema, kuondoa vikwazo kwa safari za kuvuka mipaka ndani ya Afrika kwa watu wenye ujuzi kunapaswa kutoa ishara ya juhudi za baadaye za kuleta matunda ya juhudi zinazoendelea za maingiliano ya watu wa bara hilo na kukabiliana na umasikini na majanga mengine ya kijamii.

Amesema, kutunga sheria rafiki za uhamiaji pia kutasaidia nchi za Afrika kufaidika kiuchumi na kijamii kutokana na uhuru wa kuvuka mipaka kwa wataalamu wa sekta mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha