Polisi nchini Zimbabwe yawashikilia watuhumiwa 4,300 katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya

(CRI Online) Machi 31, 2023

Polisi nchini Zimbabwe imekamata zaidi ya watu 4,300 wanaoshukiwa kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya tangu nchi hiyo ilipotangaza kuanza kwa operesheni dhidi ya dawa za kulevya.

Jumatatu wiki hii, polisi walimkamata mwanamume mmoja katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe wakati akijaribu kusafirisha kilogramu 21 za dawa za kulevya aina ya crystal meth na kilo moja ya dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya dola za kimarekani 320,000 kwenda mjini Manila, Ufilipino.

Watu wengine kadhaa wamekamatwa katika uwanja huo wa ndege mkubwa zaidi nchini Zimbabwe wakijaribu kusafirisha dawa za kulevya na dawa zingine haramu nje ya nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha