China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono Afrika katika kuongoza masuala yake ya amani na usalama

(CRI Online) Machi 31, 2023

Mwakilishi maalum wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika, Bw. Liu Yuxi ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuiunga mkono Afrika katika kuongoza masuala yake ya amani na usalama.

Bw. Liu amesema hayo kwenye mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu “Kunyamazisha milio ya bunduki barani Afrika” uliofanyika jana Alhamisi, na kuongeza kuwa, utulivu na ustawi wa dunia hauwezi kupatikana bila ya amani na maendeleo barani Afrika.

Amesema kutokana na hali mpya, Baraza la Usalama linapaswa kufikiria kwa kina njia za kuisaidia Afrika kukabiliana na changamoto mbalimbali na kushughulikia vyanzo vya migogoro.

Bw. Liu ametoa mapendekezo manne, ambayo ni kuisaidia Afrika kuongoza katika mambo yake ya amani na usalama, kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa usalama wa nchi za Afrika, kuisaidia Afrika kupata maendeleo endelevu, na kuunga mkono juhudi za pamoja za kujiendeleza barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha