China yapinga vikali aina yoyote ya mawasiliano rasmi kati ya Marekani na upande wa Taiwan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2023

BEIJING- China inapinga vikali na kulaani uratibu wa Marekani kwa kile kinachoitwa "safari ya kuunganisha" ya kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen kupitia Marekani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema Alhamisi, na kuongeza kuwa China italinda kithabiti mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi yake.

Msemaji huyo ameeleza msimamo huo kwenye mkutano na wanahabari wakati akijibu swali kuhusu kile kinachoitwa kituo cha muda katika nchi ya Marekani cha safari ya Tsai.

Amesema China inapinga vikali aina yoyote ya mawasiliano rasmi kati ya Marekani na upande wa Taiwan.

"Tunapinga kwa uthabiti ziara yoyote ya kiongozi wa upande wa Taiwan nchini Marekani kwa jina lolote au kwa kisingizio chochote, na tunapinga vikali serikali ya Marekani kuwa na aina yoyote ya mawasiliano rasmi na upande wa Taiwan," amesema.

Amebainisha kuwa kwa kupuuza upingaji mkali na tahadhari ya China ya mara kwa mara, Marekani imesisitiza kuratibu kile kinachoitwa "safari ya kuunganisha" ya Tsai kipitia nchini humo.

"China inapinga vikali na kulaani hilo," amesema.

Ameeleza kuwa Marekani na uongozi wa Taiwan walifanya uratibu kwa Tsai kujihusisha na shughuli za kisiasa nchini Marekani na kuliweka kama "safari ya kuunganisha" ili kupandisha mabadilishano rasmi na uhusiano mkubwa na upande wa Taiwan.

"Hii inakiuka sana kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, inaathiri mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya China na kutuma ujumbe usio sahihi kwa makundi yanayotaka 'Taiwan ijitenge' na China," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha