Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akutana na mwenzake wa Dominica

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang akikutana na mwenzake wa Dominica Vince Henderson huko Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 30, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

BOAO, Hainan - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amekutana na mwenzake wa Dominica Vince Henderson siku ya Alhamisi huko Boao, Mkoa wa Hainan, na kuahidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Qin amesema kuwa Dominica ni rafiki na mshirika mwenzi mzuri wa China katika eneo la Caribbean.

“China iko tayari kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Dominica mwaka ujao kwa kuimarisha mabadilishano ya pande mbili kati ya nchi hizo mbili katika pande zote, kuimarisha mabadilishano ya watu na ya kitamaduni, kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi, na kuhimiza Uhusiano wa China na Dominica kufikia kiwango kipya,” Qin amesema.

Amesema China inathamini uungaji mkono wa Dominica kwa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na inakaribisha ushiriki wake wa dhati kwenye Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.

Kwa upande wake Henderson amesema Dominica inafuata kwa dhati kanuni ya kuwepo kwa China moja na iko tayari kuimarisha ushirikiano na China katika sekta za kilimo, elimu, afya na mabadiliko ya tabianchi, na kuzidisha mabadilishano na ushirikiano kati ya Jumuiya ya Caribbean na China.

Ameongeza kuwa Dominica inaunga mkono na iko tayari kujiunga na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia ili kufanya kazi na China katika kukuza mabadilishano na kujifunza kwa pamoja kati ya ustaarabu tofauti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha