Waziri Mkuu wa China Li Qiang akutana na wanaviwanda na wafanyabiashara wa ndani na nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2023

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na wajumbe wa sekta za viwanda na biashara wa ndani na nje wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2023 huko Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 30, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

BOAO, Hainan - Waziri Mkuu wa China Li Qiang Alhamisi amekutana na wajumbe wa sekta za viwanda na biashara wa ndani na nje wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2023 huko Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China.

Baada ya kusikiliza risala za wajumbe hao, Waziri Mkuu amewashukuru kwa dhati kwa uungaji mkono wao kwa maendeleo ya China, pamoja na mchango wao wenye manufaa.

“Kampuni za aina zote, zikiwemo kampuni zinazowekezwa na mitaji kutoka nje ya China, zimeshuhudia na kuchangia ukuaji wa haraka wa uchumi na utulivu wa muda mrefu wa kijamii wa China,” Waziri Mkuu Li amesema.

Ameelezea matumaini yake kwamba wanaviwanda na wafanyabiashara wote watabeba jukumu kubwa katika kuongeza kujiamini na kuboresha matarajio.

“Ikumbukwe kwamba licha ya matatizo ya sasa, mwelekeo wa kihistoria wa utandawazi wa uchumi hautabadilika, misingi thabiti ya maendeleo ya uchumi wa China haitabadilika, mwelekeo wa jumla wa mageuzi na kufungua mlango hautabadilika, na nguvu bora za China za soko kubwa na mfumo kamili wa viwanda hautabadilika” amesema Waziri Mkuu Li.

Amesema kuwa hatua thabiti za maendeleo ya kisasa ya China zitaleta fursa nyingi zaidi za biashara na manufaa ya maendeleo kwa nchi kote duniani, na kuleta uhakika mkubwa katika uchumi wa Dunia.

Amesisitiza kuwa serikali ya China itaendelea kuweka mazingira mazuri na huduma bora kwa maendeleo ya kampuni mbalimbali, kudumisha utulivu wa kiwango katika sera yake ya uchumi mkuu, kuchukua hatua kubwa zaidi ya kuoanisha sheria za viwango vya juu za kimataifa za uchumi na biashara, na kuweka mazingira ya biashara yenye hadhi ya kimataifa ambayo yana mwelekeo wa soko, yanayotilia maanani soko, sheria na ya kimataifa.

"Kuwekeza nchini China ni sawa na kuchagua maisha bora ya baadaye," Waziri Mkuu Li amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha