Bandari ya mpakani ya Xinjiang yaripoti kuongezeka kwa usafiri wa treni za mizigo kati ya China na Ulaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 04, 2023

https://english.news.cn/20230403/4dffb95a55e645bda91f07438b06e42a/202304034dffb95a55e645bda91f07438b06e42a_452ba414-2923-44f9-b391-24964efb955b.jpg

Picha hii iliyopigwa Septemba 10, 2022 ikionyesha treni za mizigo zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya katika Bandari ya Alataw Pass, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China (Picha na Chen Qian/Xinhua)

URUMQI - Alataw Pass, bandari kuu ya reli katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China, imeshughulikia safari 1,588 za treni za mizigo kati ya China na Ulaya katika robo ya kwanza mwaka huu, ikiweka rekodi ya ongezeko la asilimia 10.35 kuliko mwaka jana, Shirika la Reli la Urumqi limesema.

Shirika hilo limesema, takriban tani milioni 3.33 za mizigo zilisafirishwa wakati wa safari hizi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.8 kuliko zile za mwaka jana.

Kuongezeka kwa usafiri wa treni za mizigo kati ya China na Ulaya kwa kiasi fulani kunatokana na ufanisi zaidi wa huduma za kupita forodha kwa treni za mizigo, shirika hilo limesema.

"Wastani wa idadi ya kila siku ya usafiri wa treni za mizigo kati ya China na Ulaya zinazohudumiwa na bandari bado ni 17 kwa sasa, ikilinganishwa na wastani wa kila mwezi wa treni 3.5 Mwaka 2012," amesema Yan Huapeng, ambaye anafanya kazi kwenye stesheni ya reli ya Alataw.

Bandari ya Alataw Pass ilishuhudia zaidi ya safari 30,000 za treni za mizigo kati ya China na Ulaya kuanzia Mwaka 2011 hadi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu. Inashughulikia kiasi kilichoongezeka cha bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, kama vile divai, chokoleti na mbolea za kemikali.

Hadi sasa, treni za mizigo za usafiri kati ya China na Ulaya zinazopita katika Bandari ya Alataw Pass zimechukua zaidi ya asilimia 30 ya treni hizo nchini China, zikifika katika nchi 19, ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Poland na Russia. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha