Tanzania kujitahidi kuulinda Mlima Kilimanjaro dhidi ya milipuko ya moto

(CRI Online) April 06, 2023

Serikali ya Tanzania imesema imeanza kuchukua hatua zinazolenga kulinda Mlima Kilimanjaro, dhidi ya matukio ya moto yanayotokea mara kwa mara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wa Tanzania Bw. Selemani Jafo amesema hatua hizo zinasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, na zinahusisha kuundwa kwa timu ya wataalamu kuchunguza chanzo cha milipuko ya moto, pamoja na kupiga marufuku shughuli za kibinadamu ikiwemo kuchoma moto kwenye mlima huo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Bw. Khamis Hamza Khamis amesema taasisi kadhaa zikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia (NM-AIST) mkoani Arusha zimeshirikishwa kwenye uchunguzi wa vyanzo vya matukio ya moto katika mlima huo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha