Kampeni ya chanjo yazinduliwa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia

(CRI Online) April 07, 2023

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema timu ya watumishi wa Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia inatoa chanjo kwa maelfu ya watoto na watu walio katika mazingira magumu ambao hawakuweza kufikiwa wakati wa mapigano katika Jimbo la Tigray.

Bw. Dujarric amesema lengo la kampeni hiyo ni kuziba pengo la kinga linalotokana na ukosefu wa huduma kutokana na mgogoro wa miaka miwili.

Wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa na Wizara ya afya ya Ethiopia, walianza kampeni ya siku 12 ya chanjo ya nyongeza dhidi ya surua.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha