Utafiti waonyesha ukatili wa kutumia bunduki nchini Marekani unakuwa hatari zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2023
Utafiti waonyesha ukatili wa kutumia bunduki nchini Marekani unakuwa hatari zaidi
Watu wakiweka mishumaa kuomboleza waathirika wa shambulizi la risasi kwenye halaiki mbele ya ukumbi wa jiji wa Monterey Park, California, Marekani, Januari 23, 2023. Mamia ya watu walikusanyika kwenye kumbukumbu ya watu 11 waliouawa na tisa kujeruhiwa kwa kupigwa risasi. (Xinhua)

NEW YORK - Idadi inayovunja rekodi ya watu waliofariki kutokana na majeraha ya bunduki nchini Marekani, na utafiti mpya unaonyesha kuwa ufyatuaji risasi kwenye halaiki unazidi kuwa wa hatari zaidi, Shirika la Habari la CNN limeripoti Jumatano.

"Waathiriwa wengi wa majeraha mabaya ya bunduki walikufa katika eneo la tukio kabla ya kutibiwa katika mazingira ya huduma za afya. Lakini hilo limezidi kuwa la kawaida katika miongo miwili iliyopita," imeeleza ripoti hiyo.

Takriban asilimia 57 ya vifo vinavyotokana na bunduki Mwaka 2021 vilitokea katika eneo la tukio, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9 tangu Mwaka 1999, kwa mujibu wa barua ya utafiti iliyochapishwa Jumatano kwenye jarida la Upasuaji la JAMA. Kwa uchambuzi huu, watafiti wametumia takwimu kutoka Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) na kuweka kando watu waliojiua na majeraha mengine yanayotokana na kujifyatulia risasi.

Karibu watu 49,000 walikufa kutokana na majeraha ya kupigwa risasi kwa bunduki nchini Marekani Mwaka 2021, takwimu za CDC zinaonyesha, ikiwa ni ongezeko ambalo halijawahi kutokea la takriban asilimia 23 kwa miaka miwili wakati wa janga la UVIKO-19, imesema ripoti hiyo.

"Na mabadiliko ya aina ya bunduki zinazonunuliwa na kutumika ni jambo kuu linalofanya ufyatuaji risasi kuwa hatari zaidi," imeongeza.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha