Utandazaji wa njia za reli inayounganisha Mji wa Tianjin na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daxing wa Beijing wakamilika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2023
Utandazaji wa njia za reli inayounganisha Mji wa Tianjin na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daxing wa Beijing wakamilika
Picha hii iliyopigwa Tarehe 25 Juni, 2019 ikionyesha jengo la abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing Daxing hapa Beijing, China. (Xinhua/Zhang Chenlin)

SHIJIAZHUANG - Kazi ya utandazaji wa njia za reli mpya inayounganisha Mji wa Tianjin wa Kaskazini mwa China na Mji wa Beijing imekamilika siku ya Alhamisi, ambayo inatarajiwa kuchochea maendeleo yaliyoratibiwa ya eneo la Beijing-Tianjin-Hebei.

Kampuni ya Beijing ya Kundi la Reli la China imesema, Reli hiyo yenye urefu wa zaidi ya kilomita 100, inaunganisha stesheni ya reli ya Tianjin Magharibi na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing Daxing, na itaanza kufanya kazi mwaka huu.

Hii ni reli ya nne ya mwendo kasi inayounganisha Beijing na Tianjin. Reli hiyo inapita katika sehemu ya njia ya reli inayounganisha Tianjin na Mji wa Baoding katika Mkoa wa Hebei, na sehemu ya reli ya kati inayounganisha Beijing na Eneo Jipya la Xiong'an la Mkoa wa Hebei. Urefu wa sehemu ya reli hiyo mpya inayojengwa ni kama kilomita 47, na kasi yake itakuwa kilomita 250 kwa saa.

Kukamilika kwa reli hiyo kutaboresha mpangilio wa mtandao wa reli katika eneo la Beijing-Tianjin-Hebei na kuchochea maendeleo jumuishi ya usafiri katika kanda hiyo, kampuni hiyo imesema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha