Rais Xi afanya mkutano wa pande tatu na Macron, von der Leyen

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2023

https://english.news.cn/20230407/7a4ed0e0c557443891e69dd8cb0b0e8f/b3d531ab5ebe4cfab1abe9b4967683b8.jpg

Rais Xi Jinping wa China akifanya mkutano wa pande tatu na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 6, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mkutano wa pande tatu na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen mjini Beijing siku ya Alhamisi.

Kwenye mkutano huo, Rais Xi amesema kuwa China na Umoja wa Ulaya (EU) zina maslahi mapana ya pamoja. Ushirikiano na misingi ya pamoja kati ya pande hizo mbili ni muhimu kuliko ushindani na migongano.

Amesema, katika Dunia iliyojaa changamoto na yenye utatanishi, China na Umoja wa Ulaya zinapaswa kuheshimiana, kuongeza hali ya kuamiana kisiasa, kuimarisha mazungumzo na ushirikiano, kudumisha amani na utulivu wa Dunia, kuhimiza maendeleo na ustawi wa pamoja, na kushughulikia changamoto za kimataifa kwa pamoja.

Huku akisisitiza uhusiano wa China na Umoja wa Ulaya haupaswi kulenga upande wa tatu au kuamriwa na upande mwingine, Rais Xi amesema kutia chumvi "demokrasia dhidi ya udikteta" na kuchochea Vita Baridi vipya kutaleta tu mgawanyiko na mapambano duniani. Amesisitiza umuhimu wa kudumisha mazingira ya wazi na ya kuaminiana kwa ushirikiano.

Rais Xi pia amezungumzia masuala mengine kadhaa ya kimataifa kama kuheshimu nafasi ya Umoja wa Mataifa katika usimamizi wa Dunia, kuoanisha Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China na Pendekezo la Global Gateway la Umoja wa Ulaya, kuimarisha na kuepusha kukata minyororo ya utoaji wa bidhaa , na kuhimiza taasisi za kifedha za kimataifa na za kibinafsi kuchangia zaidi katika kutekeleza Mpango wa Kusimamisha Ulipaji Madeni wa G20 kwa nchi zinazoendelea.

Rais Xi pia akizungumzia suala la Taiwan, amesisitiza kuwa ni kiini cha maslahi ya China. Serikali ya China na wananchi wake kamwe hawataruhusu mtu yeyote kufanya mabishano kuhusu kanuni ya kuwepo kwa China moja.

Kwa upande wake, von der Leyen akiipongeza China kwa kuandaa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai (COP15) na juhudi za China za kupunguza utoaji wa kaboni, ameeleza kuwa EU inaheshimu historia na utamaduni wa China. Mazungumzo ya ukweli na ya kiujenzi na China na maendeleo endelevu ya uhusiano wa EU na China ni muhimu kwa amani na utulivu barani Ulaya.

Naye Macron ameeleza kuwa katika Dunia iliyojaa sintofahamu, Umoja wa Ulaya na China zinahitaji kuimarisha mazungumzo na kubadilishana mawazo kwa kuheshimiana, uwazi na unyenyekevu.

https://english.news.cn/20230407/7a4ed0e0c557443891e69dd8cb0b0e8f/47e071ebcf36448ba1cebd8c3758096c.jpg

Rais Xi Jinping wa China akifanya mkutano wa pande tatu na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 6, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)

https://english.news.cn/20230407/7a4ed0e0c557443891e69dd8cb0b0e8f/c3bb5f9cfb7a43dc837f7773691b28e8.jpg

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 6, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

https://english.news.cn/20230407/7a4ed0e0c557443891e69dd8cb0b0e8f/f659b806755346ea88c150231588a871.jpg

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 6, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha