Tamasha la 40 la Kitamaduni la Maua ya Peony la Luoyang lafunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2023

Tamasha la 40 la Kitamaduni la Maua ya Peony la Mji wa Luoyang wa China limefunguliwa usiku wa tarehe 8 na litafanyika hadi tarehe 23, Aprili. Kipindi cha kutazama maua kitaendelea hadi tarehe 5, Mei. Hivi sasa, bustani zenye mapambo ya maua ya peony katika eneo la katikati la mji wa Luoyang zimeingia katika kipindi ambacho maua ya peony yamechanua kikamilifu, na peony za kila aina na rangi mbalimbali zimechanua vizuri. Hapo ndipo wakati mzuri wa kutazama maua hayo yanayopendeza.

Hafla ya ufunguzi wa tamasha hilo ilionyesha hali ya kipekee ya Luoyang kwa hadhira huku ikiifanya hadhira kuhisi haiba ya kitamaduni ya kuchanganyika kwa utamaduni wa kale na wa kisasa wa Luoyang.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha