Iran yasema kupunguza ushawishi wa dola ya Marekani kutapunguza ubabe wa Magharibi juu ya uchumi wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2023

https://english.news.cn/20230410/50ef7f102aa7490d9d27a306402779aa/2023041050ef7f102aa7490d9d27a306402779aa_6fff0a1c-8451-4c36-a932-5dfa3836dcec.jpg

Mtu akipita ofisi ya kubadilisha fedha za kigeni Cairo, Misri, Desemba 25, 2022. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

TEHRAN - Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran (SNSC) Ali Shamkhani amesema Jumapili kwamba kupunguza ushawishi wa dola ya Marekani kwenye biashara ya kikanda na kimataifa kutapunguza ubabe wa nchi za Magharibi juu ya uchumi wa Dunia.

Shamkhani ameyasema hayo kwenye mkutano wake na Msaidizi wa Rais wa Russia Igor Levitin katika Mji Mkuu wa Iran, Tehran, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Irani la Nour lenye uhusiano na SNSC.

Kwenye mkutano huo, Shamkhani amesema mchakato wa kupunguza nguvu ya dola kwenye miamala ya kikanda na kimataifa umeshaanza, akibainisha kuwa nchi nyingi zinaingia kwenye mkondo huo.

Ametaja mipango iliyokamilishwa kati ya Iran na Russia katika eneo la miamala ya fedha na benki kama njia "ifaayo" ya "kuangamiza vikwazo haramu vya Magharibi kushindwa."

Shamkhani ameeleza kuridhishwa na kuboreshwa kwa kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Iran na Russia katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, na kuashiria haja ya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kiuchumi ya pamoja.

Kwa upande wake, Levitin amesema Moscow iko tayari kufanya uwekezaji katika sekta tofauti za kiuchumi za Iran, zikiwemo zile zinazohusu viwanda vya chuma, mafuta na petrokemikali.

Iran na Russia, zote chini zilizowekewa vikwazo na Marekani, zimekuwa zikipanua uhusiano wao wa kisiasa na kiuchumi ili kukabiliana na hatua za Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha