Mkurugenzi mkuu wa WTO asema China inaunga mkono mfumo wa biashara wa pande nyingi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2023

https://english.news.cn/20230411/9774ff9c59f140439ea6b8fed443a52d/202304119774ff9c59f140439ea6b8fed443a52d_0d074861-4d39-40db-9bd7-b41a29ca8192.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala akizungumza kwenye Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa WTO (MC12) huko Geneva, Uswisi, Juni 15, 2022. (WTO/ Xinhua)

GENEVA - Kwenye mahojiano maalum na Shirika la Habari la China, Xinhua hivi majuzi, mkurugenzi mkuu wa WTO Bi.Ngozi Okonjo-Iweala alisema, China imekuwa muungaji mkono mkubwa wa mfumo wa biashara wa pande nyingi, na kama nchi yenye uchumi muhimu kwa Dunia, mchango wa China katika mfumo wa biashara huria na ulio wazi ni muhimu sana, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) .

Okonjo-Iweala amesema Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa WTO (MC12) uliofanyika Juni 2022 ulifanikiwa na "China ilitoa mchango muhimu sana katika hilo."

Mkutano wa 13 wa Mawaziri (MC13) utafanyika Februari 2024, na "tunatumai utakuwa na mafanikio sawa, lakini utahitaji kila nchi mwanachama wa WTO, ikiwa ni pamoja na China, kufanya kazi pamoja," ameongeza.

Ukiungwa mkono na sheria na kanuni za WTO, mfumo wa biashara wa pande nyingi umetoa matokeo mazuri kwa Dunia, amesema mkurugenzi mkuu huyo.

Ametoa wito kwa nchi wanachama wa WTO kuimarisha mfumo wa biashara wa pande nyingi. "Siyo wakati wa kugawanyika katika vikundi tofauti vya biashara na tunapaswa kuepuka hatua za kujilinda kiuchumi," amesema.

Kwa mujibu wa takwimu za biashara za kila mwaka za WTO na ripoti ya mtazamo iliyotolewa wiki iliyopita, biashara ya kimataifa itapata ongezeko la asilimia 1.7 Mwaka 2023, ambalo ni zaidi kuliko asilimia 1.0 lililokaridiwa mwezi Oktoba mwaka jana. Kama "mchangiaji mkuu" katika ongezeko hili, marekebisho ya China ya hatua zake za UVIKO-19 yanatarajiwa kuhimiza biashara ya kimataifa, ripoti hiyo imesema.

"Tunataka China kufanya vizuri katika biashara, ili nchi nyingine zinazoendelea... kwa mfano nchi za Afrika, ziweze kufanya vizuri," amesema.

https://english.news.cn/20230411/9774ff9c59f140439ea6b8fed443a52d/202304119774ff9c59f140439ea6b8fed443a52d_1d733ee7-c3f3-4ef5-b532-2b2591a6696b.jpg

Nembo ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) ikionekana Geneva, Uswisi, Tarehe 5 Aprili 2023. (Xinhua/Lian Yi)

https://english.news.cn/20230411/9774ff9c59f140439ea6b8fed443a52d/202304119774ff9c59f140439ea6b8fed443a52d_fd68aa62-48a4-4212-9a23-71ead97dee91.jpg

Picha hii iliyopigwa Tarehe 13 Machi 2023 ikionyesha kituo cha kontena cha Bandari ya Taicang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Bo)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha