Jiko la hisani la Misri laendelea kutoa milo bila malipo wakati wa Mfungo wa Ramadhani wakati wa mfumuko wa bei

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2023

https://english.news.cn/africa/20230411/55452789423e494e8db668fef0fcb6f5/02330d7fcaab437ca12d154e58a42516.jpg

Watu wa kujitolea wakiweka milo ya iftar kwenye boksi za kubeba vyakula nje ya Jiko la Al-Rahman huko Cairo, Misri, Tarehe 9 Aprili 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

CAIRO - Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wenye shughuli nyingi sana kwa Jiko la Al-Rahman la Misri, ambapo kutokea hapo maelfu ya milo, yote bila malipo, hutayarishwa na kupelekwa kwa sehemu mbalimbali nchini Cairo kila siku.

Katika mwezi huu mtukufu, Waislamu hufunga kutoka alfajiri hadi jua linapozama, bila kula au kunywa chochote. Jiko la Al-Rahman hutoa milo ya iftar bila malipo wakati wa machweo (kumaliza funga ya siku) kwa watu waliofunga ambao hawawezi kumudu mlo bora katika zaidi ya maeneo 30 huko Cairo.

Mohamed Gamal Basiouny, mhandisi na mkandarasi aliyeanzisha jiko hilo la hisani miaka saba iliyopita, anasema kuwa kuandaa milo mingi kila siku ni "changamoto," lakini inafaa juhudi zote zikichochewa na hisani, ukarimu na upendo kwa wengine.

"Kila siku ni changamoto, kwa jiko kuandaa takriban milo 7,000 kila siku kwa gharama ya takriban pauni 350,000 za Misri (zaidi ya dola za Kimarekani 11,000). Ni vigumu kukusanya pesa nyingi sana kila siku, lakini tulifanikiwa," Basiouny, aliyepewa jina la utani na marafiki zake la Jimmy, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Jimmy na marafiki zake huchangia katika shughuli hiyo ya hisani, na pia huwahimiza wengine kuchangia. Baadhi ya wafadhili hutoa viungo vya chakula huku wengine wakichangia pesa.

"Zaidi ya watu 300 au 400 wanafanya kazi jikoni kila siku. Wote ni watu wa kujitolea. Ni wapishi 17 pekee wanaolipwa, lakini malipo yao ni madogo kuliko juhudi wanazofanya wanapofanya kazi usiku kucha," ameongeza.

Ahmed Samir Mansour, mmiliki wa kampuni ya kemikali inayohusika na manunuzi na ukusanyaji wa michango kwa kuendesha hisani hiyo alisema kuwa, licha ya mfumuko wa bei wa juu na kupanda kwa bei nchini Misri, Jiko la Al-Rahman halikupunguza idadi ya milo yake ya kila siku ya iftar.

"Katikati ya kupanda kwa bei, idadi ya milo yetu ya kila siku ni sawa au hata imezidi ile ya mwaka jana," Mansour amesema.

"Ninawasihi watu wote kufanya hisani kama hizo. Ni jambo bora zaidi ambalo mtu anaweza kufanya," ameongeza.

https://english.news.cn/africa/20230411/55452789423e494e8db668fef0fcb6f5/ab78ce3050a346d3886882a9b95bf5cb.jpg

Watu wa kujitolea wakifunga milo ya iftar nje ya Jiko la Al-Rahman mjini Cairo, Misri, Tarehe 9 Aprili 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

https://english.news.cn/africa/20230411/55452789423e494e8db668fef0fcb6f5/37a6666dfe814008aa69902a3d50cd18.jpg

Watu wa kjitolea wakitayarisha milo ya iftar kwenye Jiko la Al-Rahman mjini Cairo, Misri, Tarehe 9 Aprili 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha