Jimu za bure zinazotumia vifaa vyenye teknolojia za akili bandia huko Xiamen, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2023

Jimu zaidi ya 30 zilizojengwa na serikali ya Mji wa Xiamen, China zimekuwa mahali pazuri pa kufanya mazoezi ya kujenga viungo vya mwili kwa wakazi wa mji huo. Wakazi wakijiandikisha kwa jina halisi, kulipa bima ya mwaka mzima kwa Yuani 10 (sawa na Tsh. 3,386), kupanga miadi mtandaoni, na kuthibitishwa nyuso zao kwenye mashine, wataingia mara moja na kufanya mazoezi bure kwenye jimu hizo zenye kutumia vifaa vyenye teknolojia za akili bandia.

Kwenye jimu hizo, hakuna wahudumu wa zamu, ni simu moja tu inahitajika kuweka miadi, kuhifadhi mavazi ya mazoezi na kufanya mazoezi. Jimu hizi zina vifaa vya kukimbilia, vya kujenga nguvu na vifaa vingine kadha wa kadha, na ukutani kuna skrini kubwa yenye kutumia teknolojia za akili bandia. Vifaa hivyo vyenye teknolojia za akili bandia vinaweza kuwafundisha wakazi kufanya mazoezi ya kujenga viungo vya mwili kwa njia sahihi, na kutuma moja kwa moja takwimu za mazoezi kwenye simu zao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha