

Lugha Nyingine
Serikali ya Yemen yakaribisha Saudi Arabia kufanya mazungumzo ya amani na kundi la Houthi
(CRI Online) April 12, 2023
Serikali ya Yemen imesema inakaribisha ujumbe wa Saudi Arabia kufanya mazungumzo ya amani na kundi la Houthi, na kutarajia matokeo mazuri. Pia imesema baada ya Saudi Arabia na Iran kurejesha kawaida uhusiano wa kidiplomasia, uwezekano wa amani nchini Yemen umekuwa mkubwa zaidi kuliko wakati wowote hapo awali.
Tarehe 9 mwezi huu, ofisa mwandamizi wa kundi la Houthi Mahdi al-Mashat alikutana na ujumbe wa Saudi Arabia uliongozwa na balozi wa nchi hiyo nchini Yemen Mohammed bin Saeed Al-Jaber huko Sana’a na kuzungumzia masuala mbalimbali yakiwemo kuhuisha makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyomaliza muda wake Mwezi Oktoba mwaka jana.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma