Uwekezaji nchini Tanzania waongezeka kwa asilimia 52.4 hadi kufikia Sh2.8 trilioni ndani ya miezi mitatu

(CRI Online) April 12, 2023

Tanzania imepata ongezeko la asilimia 52.4 la uwekezaji katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kutokana na kuimarika kwa mazingira ya biashara.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kuanzia Mwezi Januari hadi Machi, Tanzania ilivutia uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 1.2 za Marekani, ikilinganishwa na dola milioni 787.4 zilizorekodiwa Mwaka 2022.

Taarifa iliyotolewa na TIC kwa vyombo vya habari imesema kuna jumla ya miradi 93 ambayo imepangwa kutengeneza nafasi za ajira zaidi ya 16, 400.

Uwekezaji mkubwa umetokana na mitaji ya ndani, ambayo imechangia dola milioni 887 au asilimia 76 ya jumla ya uwekezaji ulioidhinishwa, na mitaji ya kigeni ilichangia dola milioni 276 ambayo ni sawa na asilimia 24. Ukuaji wa uwekezaji wa ndani ulichangiwa zaidi na sekta ya ujenzi ambayo ilikuwa na ongezeko lenye thamani ya dola za Marekani milioni 333.2.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha