Biashara ya nje ya China yarejea katika ukuaji wake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2023

Picha hii iliyopigwa Tarehe 25 Februari 2023 ikionyesha Gati la Makontena katika Bandari ya Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha hii iliyopigwa Tarehe 25 Februari 2023 ikionyesha Gati la Makontena katika Bandari ya Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

BEIJING - Biashara ya nje ya China imeanza kwa utulivu Mwaka 2023, huku jumla ya uagizaji wa bidhaa na mauzo ya nje ikiongezeka kwa asilimia 4.8 kuliko ile ya robo ya kwanza ya mwaka jana, na hivyo kubadili mwelekeo wa kushuka kwa asilimia 0.8 katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, takwimu kutoka Idara Kuu ya Forodha ya China (GAC) zimeonyesha Alhamisi.

Biashara ya nje ya China imeimarika zaidi katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Baada ya kushuka kwa asilimia 7 kuliko ile ya Mwezi Januari wa mwaka jana kutokana na likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, iliimarika na kupanuka kwa asilimia 8 Mwezi Februari, na kuongezeka kwa asilimia 15.5 Mwezi Machi mwaka huu.

Takwimu za forodha zimeonesha kuwa, kasi ya ongezeko la robo ya kwanza ilifikia asilimia 2.6 zaidi kuliko ile ya robo ya nne ya mwaka jana.

"Biashara ya nje ya China imeonyesha uhimilivu katika robo ya kwanza. Ukuaji thabiti umeweka msingi wa kuhimiza utulivu na kuboresha ubora wa biashara ya nje kwa mwaka mzima," amesema Lyu Daliang, Ofisa wa Idara Kuu ya Forodha ya China (GAC).

Katika kipindi hiki, Nchi za Ushirikiano wa Asia Kusini Mashariki (ASEAN) zimeendelea kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa China. Biashara ya China na nchi za ASEAN ilipanda kwa asilimia 16.1 kuliko mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.3 zaidi ya kiwango cha jumla cha ukuaji wa biashara nchini humu.

Pia biashara katika nchi za Ukanda Mmoja na Njia Moja nayo imeshuhudia ongezeko la asilimia 16.8.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha