UNCTAD: Kuongezeka kwa riba kupunguza zaidi ya dola bilioni 800 ya mapato ya nchi zinazoendelea

(CRI Online) April 14, 2023

Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imekadiria kwamba viwango vya juu vya riba duniani vitapunguza zaidi ya dola bilioni 800 katika mapato ya nchi zinazoendelea katika miaka ijayo.

Imeonya kuwa nchi zinazoendelea zinakumbwa na taabu wakati msukosuko wa fedha ukiongezeka na kasi ya ukuaji wa uchumi duniani ikipungua. Jumla ya ongezeko la Pato la Uchumi wa Dunia (GDP) la Mwaka 2023 linakadiriwa kuwa asilimia 2.1 tu ambapo ukuaji wa uchumi katika sehemu kubwa ya dunia utapungua ikilinganishwa na wakati wa kabla ya janga la COVID-19.

Shirika hilo limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuipa kipaumbele cha juu ajenda ya kusaidia nchi zinazoendelea ikiwemo kufanya mageuzi ya mfumo wa madeni duniani, kuongeza ukwasi na kutunga sera na kanuni za kifedha zilizo kamili na himilivu zaidi kwa uchumi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha