Maua ya kipekee ya peony yalindwa na walinzi wenye mapanga kwa masaa 24 kwa siku huko Luoyang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2023

Maua ya kipekee ya peony yanayoitwa "Yinsiguanding" yamechanua kikamilifu katika Bustani ya Mimea ya Masalio ya Mji Mkuu wa Enzi za Sui na Tang huko Luoyang, Mkoa wa Henan wa China hivi karibuni, na yanavutia watalii wengi.

Bustani hiyo imewapa majukumu walinzi wengi wanaovalia mavazi ya kale wakiwa na mapanga ili kulinda maua ya peony na kuweka utaratibu kwa zamu ya masaa 24 kwa siku. Watalii watagawanywa katika vikundi vya watu watano, na kila kikundi kinaruhusiwa kutazama maua hayo kwa sekunde 30 tu.

Maua ya peony ya aina hiyo huchanua kwa siku 10.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha