Bustani ya Kimataifa yenye njia za pampu kufunguliwa Shenyang China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2023
Bustani ya Kimataifa yenye njia za pampu kufunguliwa Shenyang China
Picha hii isiyo na tarehe ikionyesha eneo la ujenzi wa Bustani ya Kimataifa ya Michezo na Burudani yenye njia za pampu ya Shenyang huko Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua)

SHENYANG - Bustani yenye njia za pampu ya kiwango cha kimataifa inatarajiwa kufunguliwa kwa umma Mwezi Mei huko Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China.

Njia za pampu ni uwanja wa michezo au vifaa vya michezo kwa waendesha baiskeli, waendeshaji vibao vya kuteleza au waendesha skuta. Kwa kutumia mikono na miguu yao, waendeshaji wanaweza kujaza upepo baiskeli, vibao au scooters zao kwa kutumia pampu zilizo karibu na njia zinazojumuisha kuruka, roller na miinuko ya pindo za kuruhusu kugeuka kwa kuzunguka juu.

Bustani ya Kimataifa yenye njia za pampu ya Shenyang iko katika Bustani ya Xihe Yougu ya Eneo la Maendeleo ya Uchumi na Teknolojia la Shenyang, ikiwa kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 7,000 za njia za pampu zinazosambaa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 18,000.

Eneo hilo la njia za pampu limegawanywa katika eneo la kiumma na eneo la kitaaluma na limezungukwa na eneo la huduma na miundombinu ya kina ya watembeleaji, ikiwa ni pamoja na maduka ya kahawa, supamaketi, maduka ya vitafunio, na eneo la maegesho.

Eneo la Maendeleo ya Uchumi na Teknolojia la Shenyang limesema, Baada ya kufunguliwa, itakuwa eneo kuu kwa wapenda michezo wa Shenyang, alama mpya ya utalii wa mjini, mapumziko na burudani, na sehemu ya kiwango cha juu kwa mashindano ya michezo ya kimataifa .

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha