

Lugha Nyingine
China na Jumuiya ya Kimataifa yataka mapigano nchini Sudan kusitishwa mara moja
![]() |
Picha hii iliyopigwa Tarehe 15 Aprili 2023 ikionyesha moshi ukifuka Khartoum, Sudan. (Picha na Mohammed Khidir/Xinhua) |
BEIJING - Mgogoro wa kijeshi wa Sudan kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka wa Kijeshi (RSF) umefuatiliwa karibu na China na jumuiya ya kimataifa, huku wito ukiongezeka wa kutaka mapigano hayo yasitishwe mara moja.
Mapigano hayo yameua takriban watu 56 hadi kufikia Jumapili jioni, na wengine 595 kujeruhiwa, mapigano hayo, ambayo yalizuka Jumamosi asubuhi na kuendelea hadi Jumapili, bado hayajaonekana kuwa na dalili ya kupoa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imezitaka pande zinazopingana nchini Sudan kusimamisha mapigano mapema, ili kuzuia hali isizidi kuwa mbaya.
Pia wizara hiyo imesisitiza kuwa, China inazitaka pande mbalimbali nchini Sudan ziimarishe mazungumzo ili kuhimiza kwa pamoja mchakato wa mpito cha kisiasa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres Jumamosi amelaani vikali kuzuka kwa mapigano hayo kati ya vikosi hivyo viwili, amesema msemaji wake.
"Katibu Mkuu anatoa wito kwa viongozi wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka na Vikosi vya Wanajeshi vya Sudan kusitisha mara moja uhasama, kurejesha utulivu na kuanzisha mazungumzo ya kutatua mgogoro uliopo," amesema Stephane Dujarric, msemaji Guterres katika taarifa yake.
Katika taarifa yake, Umoja wa Afrika (AU) umesema "unaendelea kufuatilia kwa karibu sana na kwa wasiwasi mkubwa maendeleo" nchini Sudan, na kuzitaka pande za kisiasa, kiraia na wanajeshi nchini humo kutafuta suluhu ya maafikiano juu ya mgogoro huo.
Misri, Qatar, Libya, Iran, Jordan, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine pia zimetaka kukoma kwa mapigano hayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma