Uchumi wa China wafufuka kwa hatua madhubuti kufuata kuongezeka kwa matarajio ya soko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2023

Picha hii iliyopigwa Februari 25, 2023 ikionyesha  magari yanayojiendesha  yakibeba makontena kwenye gati la kontena la kiotomatiki kwenye Bandari ya Qinzhou, katika Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, nchini China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha hii iliyopigwa Februari 25, 2023 ikionyesha magari yanayojiendesha yakibeba makontena kwenye gati la kontena la kiotomatiki kwenye Bandari ya Qinzhou, katika Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, nchini China. (Xinhua/Zhang Ailin)

BEIJING - Dalili nyingi zinaonyesha kuwa uchumi wa China umekuwa ukiimarika huku kukiwa na msukumo mkubwa na imani iliyongezeka ya soko tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na wachambuzi wanatarajia uwezekano zaidi wa ukuaji wa uchumi katika robo zijazo za mwaka.

Biashara ya nje na ukuaji wa mikopo kwa pamoja vimevuka makadirio ya soko katika robo ya kwanza, na shughuli za utengenezaji bidhaa na matumizi vimeendelea kuimarika, takwimu rasmi za serikali zimebainisha.

Taasisi ya Utafiti ya Benki Kuu ya China imesema, kadiri athari za UVIKO-19 zilivyopungua kwa kiasi kikubwa, sera za uimarishaji wa uchumi ziliwekwa mapema, uchumi wa China uliendelea kuimarika katika robo ya kwanza, na imani ya soko na matarajio yaliongezeka kwa kiasi kikubwa.

Takwimu kutoka Idara Kuu ya Forodha ya China wiki iliyopita zinaonyesha kuwa biashara ya nje imekuwa ikiboreka katika miezi mitatu iliyopita. Baada ya kushuka kwa asilimia 7 kutoka kwenye kiwango cha Mwezi Januari mwaka jana kutokana na likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, iliimarika na kupanuka kwa asilimia 8 Mwezi Februari, na iliongezeka kwa asilimia 15.5 Mwezi Machi.

Kwa upande wa sekta ya fedha, ukuaji wa mikopo inayotokana na fedha ya yuan ulifikia yuan trilioni 10.6 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la yuan trilioni 2.27 kuliko mwaka uliopita, wakati ukusanyaji wa mitaji kwenye jamii ulifikia yuan trilioni 14.53 katika robo ya kwanza ikiwa ni ongezeko la yuan trilioni 2.47 kuliko lile la kipindi kama hicho mwaka jana.

Shughuli za utengenezaji bidhaa za China zilidumisha upanuzi wake kwa miezi mitatu mfululizo kufikia Machi, na faharisi ya wasimamizi wa ununuzi (PMI) kwa viwanda vya utengenezaji bidhaa vya China ilifikia 51.9, na PMI kwa viwanda visivyo vya utengenezaji bidhaa ilifikia 58.2.

“Mwezi Machi mwaka huu, kasi ya ukuaji wa mauzo ya nje ya nchi zenye biashara kubwa ya nje duniani iliendelea kupungua. Kinyume chake, mauzo ya nje ya China bado yalipata ukuaji licha ya msingi wa juu mwaka wa 2022, na kiwango cha ukuaji kilizidi matarajio ya soko,” amesema Wang Jing, mtafiti katika Taasisi ya Utafiti ya Benki ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha