

Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akutana na mwenzake wa Laos
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akikutana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos Saleumxay Kommasith Mjini Beijing, China, Aprili 17, 2023. (Xinhua/Liu Weibing)
Beijing – Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang amekutana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos Saleumxay Kommasith mjini Beijing siku ya Jumatatu.
Ding, ambaye pia Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ametoa wito kwa nchi zote mbili kufanya kazi kwa mwelekeo thabiti katika ujenzi wa jumuiya ya China na Laos yenye mustakabali wa pamoja, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
Ding amesema, China iko tayari kufanya kazi pamoja na Laos ili kuifanya reli ya China na Laos kuwa yenye kuleta manufaa zaidi, kuendelea kuimarisha mabadilishano kati ya watu na ya kitamaduni, kulinda kwa pamoja ustawi na utulivu wa kikanda, na kusukuma mbele mafanikio mapya katika ushirikiano wa kivitendo.
Kwa upande wake, Saleumxay ameishukuru China kwa uungaji mkono na usaidizi wake kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Laos, na kuongeza kuwa Laos inaunga mkono kithabiti na kushiriki kikamilifu katika mipango na dhana kuu zinazopendekezwa na China.
Saleumxay amesema Laos iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kivitendo wa pande mbili katika sekta mbalimbali, kujenga vyema jumuiya ya Laos na China yenye mustakabali wa pamoja, na kuhimiza maendeleo ya lengo la ujamaa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma