Spika wa Bunge la Umma la China afanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Slovakia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 19, 2023

https://english.news.cn/20230418/3f9416c49588480ea7e19e3448b328e3/d8a5ade085714660b1bc65c263ed5587.jpg

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Boris Kollar, Spika wa Bunge la taifa la Slovakia, mjini Beijing, China, Aprili 18, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

BEIJING - Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China (NPC), amefanya mazungumzo na Boris Kollar, Spika wa Bunge la taifa la Slovakia, Jumanne hapa Beijing.

Akipongeza urafiki wa tangu zamani kati ya nchi hizo mbili, Zhao amesema katika miaka ya hivi karibuni, chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Ushirikiano kati ya China na Ulaya ya Kati na Mashariki (CEE), China na Slovakia zimepata matokeo chanya ya ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, sayansi na teknolojia, utalii, utamaduni, na mafungamano ya mawasiliano, na kuleta manufaa kwa watu wa pande hizi mbili.

Zhao ameongeza kuwa China iko tayari kushirikiana na Slovakia kwa dhati kuupeleka mbele, kudumisha na kuendeleza urafiki wao wa jadi.

Amezitaka pande hizo mbili kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji na usafirishaji, akisema, China inakaribisha kampuni za Slovakia kupanua soko nchini China kupitia majukwaa yakiwemo Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China na Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje wa Bidhaa ya China, na anatumai upande wa Slovakia utatoa mazingira ya biashara ya haki, usawa, na yasiyo na upendeleo kwa kampuni za China.

Kwa upande wake Kollar huku akiitaja China kuwa mshirika muhimu, amesema nchi hizo mbili zina msingi mpana na uwezo mkubwa wa ushirikiano. Amesema, Dunia ina rangi nyingi, na hakuna mtu ambaye yuko katika nafasi ya kutafuta mapambano au kufundisha wengine kutokana na tofauti za mifumo ya kisiasa.

https://english.news.cn/20230418/3f9416c49588480ea7e19e3448b328e3/c6e1f350be494b8a85cfa0fe011dbd58.jpg

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Boris Kollar, Spika wa Bunge la taifa la Slovakia, mjini Beijing, China, Aprili 18, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha