Umoja wa Mataifa wafuatilia ripoti za Marekani kuingilia mawasiliano ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 19, 2023
Umoja wa Mataifa wafuatilia ripoti za Marekani kuingilia mawasiliano ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Picha iliyopigwa Septemba 14, 2020 ikionyesha mwonekano wa nje wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. (Xinhua/Wang Ying)

UMOJA WA MATAIFA - Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema Jumanne kwamba shirika hilo limeeleza rasmi kwa Marekani ufuatiliaji wa karibu wa chombo hicho cha Dunia juu ya ripoti za uingiliaji wa mawasiliano binafsi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

"Umoja wa Mataifa umeeleza rasmi kwa nchi mwenyeji juu ya ufuatiliaji wake wa karibu kuhusu ripoti za hivi karibuni kwamba mawasiliano ya katibu mkuu na maofisa wengine wakuu wa Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifuatiliwa na kuingiliwa na serikali ya Marekani," amesema Dujarric.

"Umoja wa Mataifa umesema wazi kuwa vitendo kama hivyo haviendani na majukumu ya Marekani yaliyowekwa kwenye Katiba ya Umoja wa Mataifa na Mkataba wa Haki na Kinga wa Umoja wa Mataifa," ameongeza.

Gazeti la Washington Post siku ya Jumatatu liliripoti kuwa kwa mujibu wa ripoti nne za siri zilizopatikana kwa gazeti hilo, Marekani ilisikiliza na kukusanya upelelezi kuhusu Guterres.

Nyaraka hizo, ambazo mbili kati yake hazijaripotiwa hapo awali, ambazo zimefanya majumuisho kuhusu mazungumzo yaliyonaswa kuhusu mawasiliano kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na maofisa wakuu wa UN na viongozi wa Dunia, gazeti hilo liliripoti.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha