Majenereta ya Umeme wa Nyuklia ya China yako kwenye safu ya mbele duniani ya usalama wa uendeshaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 20, 2023
Majenereta ya Umeme wa Nyuklia ya China yako kwenye safu ya mbele duniani ya usalama wa uendeshaji
Tarehe 25, Machi, majenereta ya kwanza ya umeme wa nyuklia ya Magharibi mwa China ya “Hualong One” yalianza kufanya kazi. Picha ilitolewa na Shirika la Nishati la General Nuclear la China.

"Majenereta ya umeme wa nyuklia ya China yanadumisha uendeshaji wa usalama na utulivu, na katika miaka 30 iliyopita, hayajatokea matukio ya uendeshaji ya ngazi ya pili au ya juu zaidi kwenye kiwango cha kimataifa cha matukio ya nyuklia na utoaji wa mionzi. Kiwango cha uendeshaji wa usalama wa majenereta ya umeme wa nyuklia kiko kwenye safu ya mbele duniani." Alisema Ye Qizhen, mtaalamu wa Taasisi ya Uhandisi ya China kwenye hafla ya uanzishaji wa shughuli ya 11 ya "Nuru Yenye Mvuto" ya kueneza ujuzi wa sayansi kuhusu nyuklia iliyofanyika tarehe 15, Aprili.

Naibu waziri wa Mazingira ya Asili, ambaye pia ni mkuu wa Idara ya Usalama wa Nyuklia ya China Dong Baotong alijulisha kwenye hafla kuwa, hivi sasa katika sehemu mbalimbali nchini China kwa jumla kuna majenereta 77 ya umeme wa nyuklia, ambayo yamedumisha rekodi nzuri ya usalama. Vyanzo laki 1.64 vya utoaji mionzi na vifaa laki 2.67 vya utoaji mionzi viko chini ya udhibiti salama, na hali ya jumla ya mazingira ya utoaji mionzi nchini China ni nzuri.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha