Uingiaji wa Uwekezaji wa moja kwa moja wa Kigeni (FDI) nchini China warekodi ukuaji thabiti katika robo ya kwanza ya Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2023

Picha hii iliyopigwa Januari 1, 2023 ikionyesha meli ya kontena ikiwa kwenye Bandari ya Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

Picha hii iliyopigwa Januari 1, 2023 ikionyesha meli ya kontena ikiwa kwenye Bandari ya Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

BEIJING - Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) katika sehemu mbalimbali nchini China umerekodi ukuaji wa kasi katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2023, ikionyesha nchi ya China yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani imeendelea kuwavutia zaidi wawekezaji wa duniani.

Wizara ya Biashara ya China imesema Alhamisi kuwa, uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni katika matumizi halisi nchini China uliongezeka kwa asilimia 4.9 kuliko ule wa mwaka jana na kufikia yuan bilioni 408.45 (kama dola bilioni 59.2 za Kimarekani) katika kipindi cha miezi ya Januari hadi Machi.

Kampuni mpya zaidi ya 10,000 zenye uwekezaji wa nchi mbalimbali zilianzishwa katika kipindi hiki, ikiwa ni ongezeko la asilimia 25.5 mwaka hadi mwaka.

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China zimeonesha kuwa, uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni katika viwanda vya teknolojia ya hali ya juu uliongezeka kwa asilimia 18 kuliko ule wa kipindi kama hicho cha mwaka uliopita.

Hasa, sekta ya utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki na simu imeshuhudia kuongezeka kwa uwekezaji wa kigeni kwa asilimia 55.7.

Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni katika huduma zinazohusiana na utafiti na maendeleo na usanifu uliongezeka kwa asilimia 24.6, wakati uwekezaji huo katika viwanda vya dawa uliongezeka kwa asilimia 20.2.

“Kumekuwa na uboreshaji endelevu katika suala la ubora na muundo wa uwekezaji huo nchini China,” amesema msemaji wa wizara hiyo Shu Jueting.

Amesema uboreshaji huo umetokana na uanzishwaji wa vituo vya Utafiti na Maendeleo (R&D) vinavyowekezwa na wafanyabiashara wa nchi za nje, juhudi za kuvutia uwekezaji katika viwanda, na orodha mpya ya tasnia nchini China kwa ajili ya kuhamasisha uwekezaji kutoka nje.

Katika kipindi hicho, uwekezaji kutoka Ufaransa na Ujerumani uliongezeka kwa asilimia 635.5 na asilimia 60.8 kuliko ule wa mwaka jana, huku ule kutoka nchi zilizo kando ya Ukanda Mmoja, Njia Moja nao uliongezeka kwa asilimia 27.8. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha