Ripoti yaonyesha Sera mpya ya China ya UVIKO imeongeza mahitaji ya kimataifa, kupunguza shinikizo la utoaji bidhaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 21, 2023

Matairi yakionyeshwa kwenye sehemu ya Mabanda ya Magari na Vipuri ya Maonyesho ya 133 ya Uagizaji na Uuzaji nje wa Bidhaa ya China, huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 15, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

HELSINKI - Taasisi ya Kazi za Utafiti wa Kiuchumi ya Finland (LABORE) imesema katika makadirio yake ya kiuchumi ya Mwaka 2023-2025 yaliyochapishwa Alhamisi kuwa, uboreshaji wa sera za China za kukabiliana na UVIKO-19 umeongeza mahitaji ya kimataifa na kupunguza vizuizi kwenye minyororo ya utoaji bidhaa.

“Wakadiriaji wengi wa kiuchumi wanatarajia uchumi wa nchi ya China kukua kwa uendelevu katika miaka ijayo kufuatia marekebisho yake ya hivi majuzi katika hatua zake za kukabiliana na UVIKO-19,” taasisi hiyo imesema.

Maendeleo chanya ya uchumi wa China yanaongeza mahitaji ya kimataifa na kupunguza shinikizo kwenye minyororo ya utoaji wa bidhaa na kuwa na mchango chanya kwa uchumi wa Dunia.

Kuhusu uchumi wa Dunia, taasisi hiyo ya makadirio ya uchumi ya Finland imesema kuwa mfumuko wa bei ulioenea na matokeo yake ya kusababisha kukazwa kwa sera za fedha kunatarajiwa kuathiri ukuaji wa uchumi wa Dunia kwa kiasi kikubwa. Kuendelea kwa vita kati ya Russia na Ukraine na kuongezeka kwa mvutano kati ya Marekani na China pia kunaongeza hali ya sintofahamu duniani.

Kwa mujibu wa mashirika makubwa ya makadirio, uchumi wa Marekani utashuka kwa kiasi kikubwa Mwaka 2023 na unatarajiwa kuimarika Mwaka 2024 na 2025. Uchumi katika eneo linalotumia fedha ya Euro, Euro Zone utakua, ingawa uchumi wa Ujerumani huenda ukadhoofika Mwaka 2023. Uchumi wa Uingereza unatarajiwa kusinyaa mwaka huu na hautaimarika kwa kiasi kikubwa Mwaka 2024.

Muonyeshaji akipanga bidhaa za sauti kwenye Mabanda ya Bidhaa za Matumizi za Kielektroniki na Upashanaji wa Habari katika Maonyesho ya 133 ya Uagizaji na Uuzaji nje wa Bidhaa ya China, huko Guangzhou, mkoani Guangdong, China, Aprili 15, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

Wanunuzi wa Uingereza wakijadiliana kuhusu biashara kwenye Mabanda ya Magari na Vipuri ya Maonyesho ya 133 ya Uagizaji na Uuzaji nje wa Bidhaa ya China, huko Guangzhou, mkoani Guangdong, China, Aprili 15, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha