

Lugha Nyingine
Russia yasema itawafukuza wanadiplomasia wa Ujerumani baada ya vitendo vya "kiuhasama" vya Ujerumani
Picha iliyopigwa Aprili 16, 2021 ikionyesha Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia huko Moscow. (Xinhua/Evgeny Sinitsyn)
MOSCOW - Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema Jumamosi kwamba imeamua "kujibu" vitendo vya "kiuhasama" vya Ujerumani na kuwafukuza wanadiplomasia wa Ujerumani kutoka Russia.
"Serikali ya Ujerumani imeamua kufukuza tena kwa wingi wafanyakazi wa ubalozi wa Russia nchini Ujerumani. Tunalaani vikali vitendo hivi vya Berlin, ambavyo vinaendelea kuharibu kwa ukaidi safu nzima ya uhusiano wa Russia na Ujerumani," wizara hiyo imesema katika taarifa yake.
Idadi ya juu ya wafanyakazi katika ujumbe wa kidiplomasia wa Ujerumani nchini Russia pia itakuwa na ukomo kwa "kiasi kikubwa”, imesema wizara hiyo, na kuongeza kuwa Aprili 5, 2023, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilimjulisha rasmi Balozi wa Ujerumani nchini Russia, Geza Andreas von Geyr juu ya uamuzi huo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani haijatoa kauli rasmi kuhusu suala hili.
Mwezi Aprili mwaka jana, Ujerumani ilitangaza kuwafukuza wanadiplomasia 40 wa Russia, na Russia ikatangaza hatua za papo kwa papo za kulipiza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma