Kusoma Dunia pamoja na Rais Xi Jinping | Mashairi ya Shaaban Robert

By Zhou Linjia, Aris, Song Ge, Ebulayi, Su Yingxiang (Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2023

Leo nitawajulisha kitabu kimoja kilichoandikwa na Shaaban Robert, mwandishi wa vitabu na mhakiki wa fasihi maarufu wa Tanzania.

“Cheka uzuie kwisha, maishayo mbio mbio. Furaha ndiyo tamasha, kiumbe aliyo nayo. Hata nyota zakumbusha, kuwa nayo hali hiyo. Mawingu yanapotenga, nyota mbinguni hucheka. Chini likashuka anga, la furaha kupeleka, Kwa wakubwa na wachanga, wapate kufurahika.”

Sentensi hizi zinatoka kwenye shairi la “CHEKA KWA FURAHA”. Sababu ya kusifiwa na kupendwa na watu wengi kwa mashairi ya Shaaban Robert ni kwamba maudhui ya mashairi yake yalionesha hali halisi ya maisha ya watu, yalieleza ufuatiliaji wake juu ya taabu za watu, na kuashiria matarajio na matumaini juu ya jamii bora.

Kujikita miongoni mwa watu, ni sawa na matakwa aliyotoa Rais Xi Jinping wa China juu ya kazi bora za fasihi na michezo ya sanaa.

Xi Jinping aliwahimiza watu wanaoshughulika na kazi hizo wakumbuke siku zote hali ya maisha ya watu, taabu na furaha walizonazo kwenye Kongamano la kazi za utunzi wa fasihi na michezo ya sanaa Mwezi Oktoba, Mwaka 2014.

Leo maelezo kuhusu kitabu yanaishia hapa. Tunatumai watazamaji wetu mnaweza kupata maarifa fulani mtakapokisoma.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha