Sekta ya utoaji huduma ya China yapata msukumo wa kuimarisha uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2023

Yu Shufen akitoa huduma ya chakula kwa wateja kwenye hosteli zake zilizoko Kijiji cha Nangou, karibu na Eneo la Burudani za Kuteleza kwenye Theluji la Beidahu, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China, Februari 11, 2023.(Xinhua/Tao Xiyi)

Yu Shufen akitoa huduma ya chakula kwa wateja kwenye hosteli zake zilizoko Kijiji cha Nangou, karibu na Eneo la Burudani za Kuteleza kwenye Theluji la Beidahu, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China, Februari 11, 2023. (Xinhua/Tao Xiyi)

BEIJING - Ikiendeshwa na uboreshaji wa hisia za watumiaji kwenye manunuzi na sera za kuhimiza uchumi, sekta ya huduma ya China inashika kasi ya ukuaji wake, na kuchangia kuimarisha uchumi kutoka kwenye athari za UVIKO-19.

Pato la huduma za ongezeko la thamani la China liliongezeka kwa asilimia 5.4 mwaka hadi mwaka katika robo ya kwanza ya Mwaka 2023, huku kasi yake ya ukuaji ikiongezeka kwa asilimia 3.1 kutoka robo ya nne ya Mwaka 2022, takwimu kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zinaonyesha.

Ahueni katika sekta ya huduma, ambayo ilichangia asilimia 69.5 ya ukuaji wa jumla wa Pato la Taifa la China (GDP) katika robo ya kwanza ya mwaka huu, imekuwa sehemu muhimu za ukuaji katika shughuli za kiuchumi za China tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kwa mujibu wa msemaji wa NBS Fu Linghui.

Sekta za kupata huduma ana kwa ana, ambazo ziliathiriwa sana na vizuizi vya UVIKO-19, hatua kwa hatua zinaanza kuimarika. Sekta ya malazi na vyakula ilipanda kwa asilimia 13.6 mwaka hadi mwaka katika robo ya kwanza, tofauti na kupungua kwa asilimia 5.8 katika robo iliyopita.

Mwenendo wa safari za abiria na uchukuzi wa bidhaa wa China unarejea haraka kwenye hali ya kawaida. Takriban safari za kitalii za ndani milioni 24 zilifanywa nchini China wakati wa mapumziko ya Siku ya Qingming, ambayo mwaka huu ilikuwa Aprili 5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.7 kutoka mwaka jana, kwa mujibu wa Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China (MCT).

China imeweka lengo la ukuaji wa Pato la Taifa la karibu asilimia 5 kwa Mwaka 2023. Mapema mwezi huu, Shirika la Fedha la Kimataifa lilikadiria ukuaji wa uchumi wa China kwa asilimia 5.2 mwaka huu, kutoka asilimia 3 mwaka jana. Wakati huo huo, Benki ya Dunia inatarajia ukuaji wa Pato la Taifa la China kuongezeka hadi asilimia 5.1 Mwaka 2023.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha